Burudani

Meneja wa zamani wa Diamond aeleza kwanini msanii huyo anazidi kufanikiwa

Meneja wa zamani wa Diamond Platnumz, Msafiri Misifa maarufu kama Papa Misifa, amesema wasanii wengi wanashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kuhifadhi wanachokipata.

Kassim Mganga na mdau wa muziki
Papa Misifa ( wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Cassim Mganga

Papa Misifa aliyewahi pia kuwa meneja wa Dully Sykes na Cassim Mganga, ameiambia Bongo5 kuwa Diamond ni msanii pekee aliyeweza kufuata mafunzo yake na ndio maana anaendelea kufanikiwa mpaka sasa.

“Tatizo kubwa wasanii sana wanapopata riziki wanashindwa kujipangilia. Na mafunzo mengi niliyompa Diamond ndo maana mpaka leo anajua kujipangilia mpaka pale alipofika. Wasanii wanashindwa kupangilia pesa zao. Tatizo wanapopata pesa wanabadilika. Ukitaka kujua tabia ya mwanadamu ngoja apate pesa ndo utajua tabia yake,” amesisitiza.

“Wasanii wengi hawalengi kufanya vitu vya maendeleo, wanalenga kufanya starehe kwenye baa. Ndio maana watu wanasema wanamuziki wa zamani wamefulia ni kweli kwa sababu hawakujipanga. Hawakutambua kesho yao, wewe unafikiri kwanini Diamond anaiogopa kesho yake? Ni kutokana na maisha yalivyo ukipata nafasi itumie ipasavyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents