Burudani

Mdogo wa kiume wa Lupita Nyong’o, Peter Nyong’o apata shavu la kwanza la kuigiza filamu ya Hollywood

Mdogo wa kiume wa mwigizaji wa Kenya, Lupita Nyong’o aitwaye Peter Nyong’o ameanza kufata nyayo za dada yake kwa kupata shavu la kuigiza kwenye filamu mpya huko Hollywood.

Lupita and Peter

Peter amepata nafasi ya kucheza kwenye filamu ya ‘Nocturnal Animals’ ya Tom Ford ambayo itatoka mwakani 2016. Hii itakuwa ndio mara yake ya kwanza kugiza kwenye filamu ya Hollywood.

“Humbled by this opportunity to work with such a phenomenal director and talented cast for my first role in a feature film. But more than anything, excited to get to work!‪” alisema Peter.

Ulimwengu ulianza kumfahamu Peter baada ya kumsindikiza Lupita kwenye tuzo za Oscar ambapo alishinda Best Supporting Actress kwenye filamu ya ‘12 Years a Slave’ na kumpa shoutout mdogo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents