Tragedy

Mdee, Mengi, Zitto Kabwe na wengine wamlilia marehemu Dr. Mvungi

Wabunge Halima Mdee na Zitto Kabwe pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi wametoa maoni yao kuhusiana kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi aliyefariki jana alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

mvungi
Picha ya Dr. Sengondo Mvungi wakati wa uhai wake.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Kifo chake kimesababisha simanzi kubwa na hivi ndivyo viongozi na watu wengine wanavyokizungumzia kifo chake.


Halima James Mdee ‏@halimamdee 1h

RIP mwalimu wangu Dr.Mvungi. Kinachoniuma zaidi wauaji wa nchi hii ,hawataacha kuangamiza roho zisizo Na hatia,wanajua hakuna wa kuwakamata!.


Reginald Mengi ‏@regmengi 1h

Tunapoomba Mungu ailaze roho ya Dr Mvungi mahali pema peponi, kwa ukatili hu watz tujiulize tumefikaje hapa na tunaelekea wapi.Dr Mvungi RIP.

Zitto Kabwe
Mwalimu Sengodo Mvungi, baba wa rafiki yangu dkt. Natujwa Mvungi, mmoja wa wataalamu mahiri wa masuala ya Katiba umetutoka ukiwa kwenye kazi ya kihistoria. Kazi ya kuandika katiba yetu. Umetangulia kabla kazi haijaisha. Ni wajibu wetu kuimaliza kazi hii kukuenzi. Tangulia baba yetu. Tangulia Mwalimu wetu. Tumshukuru mola kwa yote.

Matukio Chuma

Dkt Sengondo mwana wa Mvungi, umekwenda, weledi wako, masomo yako, ucheshi wako, mafunzo yako, yalitufanya sharia ihusuyo ama zihuzuzo Katiba kwa wingi wake uelewa na zako bashasha hatukuhuisha bali tulistawisha, ASANTE MKUU,

Wala sisemi pumzika pema maana mapakashume yaliyoamua ama kutumwa kukumaliza labda ukiyakumbuka usiyape usingizi Mkuu, imekuwa nchi isiyomithilika iliyojaa chuki ikachukwikwa na wahusika nao kama vile pilipili, ndimu na limao zimewatwika, Dkt, Mkuu, Kamanda, Mlezi, Baba, Mtaaluma, umekwenda lakini kwa hakika kishujaa kwa maana wangekupinga kwa hoja si kwa mapanga wamegeuka MAHOKA,

Waache wafumbe macho, waache wajifanye wanaangalia lakini eti hawaoni, wakijifanya tafakuri lakini hawana fikiri, YALAITI WAKATI MWINGINE LABDA 2015 INGALIKUWA KESHO,

Ndimi Mwanafunzi wako,
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

Mungu ailaze roho ya marehemu Dr.Mvungi mahali pema poponi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents