Habari

Mchungaji Gwajima adai mtoto aliyejifungua Flora Mbasha si wake

Siku chache baada ya kuzagaa picha zinazodai ni za mtoto wa muimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha na kuwepo tetesi kuwa huenda ni mtoto wa mchungaji Josephat Gwajima, wawili hao wamelazimika kuzungumza.

GWAJIMA

Akizunguza na gazeti la Mtanzania jana, kusuhu picha za mtoto mchanga zilizozagaa, Mchungaji Gwajima, alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora.

“Hahaha… si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu, wakati mwingine mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.

“Awali niliwaza kuwashitaki (alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na Flora) wanaoeneza uzushi huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’ (haina mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,” aliongeza Gwajima.

Hata hivyo Gwajima alisema hakujua kama Flora ni mjamzito wakati anaenda kuomba msaada kanisani kwake.

“Mimi sikujua kama alikuwa mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndio nazisikia kwako. Hapa nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam,” alisema na kuongeza:

“Sasa kama mtu una wasiwasi na mtoto si ukapime DNA ili upate uhakika? Hii ni habari ya kutaka tu kulichafua kanisa na huduma,” alisisitiza.

Pia kwa upande wa Flora alisema “Siko tayari kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa. Yeye ana jeuri ya pesa ndo maana anafanya haya yote lakini mimi ninasimama na Mungu wangu na ninajua Mungu atanipigania,” alisema Flora.

Alipoulizwa kuhusu hali ya mtoto wake mchanga, alisema “Mtoto hajambo, lakini mtoto anayesambazwa kwenye mitandao sio wangu, na hizo picha nyingine nafikiri ni za kutengeneza tu,” alisema Flora.

Katika hatua nyingine gazeti la Mtanzania lilimtafuta Emmanuel Mbasha, ili kuzungumzia suala hilo, licha ya kupokea simu yake ya kiganjani, aliishia kusema yuko njiani hivyo apigiwe baadaye.

Hata alipopigiwa baadaye, aliendelea kusema kuwa atafutwe baadaye na wala hakujibu ujumbe wa simu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents