Michezo

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Godfrey Bonny afariki dunia

By  | 

Kiungo wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefariki dunia alhamisi hii huko nyumbani kwao Mbeya.

Mchezaji huyo alikuwa amelazwa kwa muda mrefu hospitali ya Rungwe-Tukuyu Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati akicheza soka, Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments