Michezo

Mchezaji afariki akisherehekea bao kwa kuruka sarakasi

Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea goli alilofunga.

page

Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kuanguka uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.

Mechi hiyo ambapo alipata jeraha la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kupitia kwa mtandao wa Facebook,uliandika: “Imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram,”.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents