Burudani

Mchekeshaji Eric Omondi amshukuru Diamond kwa kumfungulia milango Tanzania!

By  | 

Erick Omondi mchekeshaji kutoka hapa nchini Kenya ambaye kwa hivi sasa anakubalika Afrika na sehemu zingine za dunia ikiwemo bara Ulaya na America, Ijumaa iliyopita ya tarehe 10 alipoalikwa kwenye kipindi cha #TheTrend kinachorushwa na kituo cha NTV na kuongozwa na mtangazaji Larry Madowo, alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye soko la Tanzania.

Omondi ambaye kipaji chake cha ucheshi kilikuzwa na mkongwe kwenye tasnia ya comedy Kenya, Daniel Ndambuki aka Churchill kwenye platform kubwa Afrika ya comedy maarufu kama Churchill-Show, anasema hana shauku na upendo na support anoyoipata kutoka kwa watanzania.

Nikinukuu baadhi ya maneno yake kwenye interview hiyo na Larry:

Larry : How did you get so wildly popular in Tanzania?

Eric : Aaah…Diamond

Larry: Aaah

Eric : I met Diamond in a two, three years in Mombasa, I had done his song …Nabeba mawe… he loved it so when we met he was like..aah we jamaa nimekeutafuta sana bana. So he invited me to one of the biggest show in that land called Zari all white part. It was huge…huge and very successful.

Larry: It was huge………

Eric : It was huge believe me…was very huge…and that was my entrance, so he told me ” I want you to be my MC at my Zari white part that like 10,000 people.

Larry: Woow!

Eric : So I saw that, nikasema ok, I started preparing and ensuring…because I knew, all the TV stations and radios will be there. ….so I went and my best.

Erick pia alichuka fursa hiyo kuwatangazia mashabiki wake wa Bongo, kuwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo, atakuwa anaanzisha Comedy TV show nchini Tanzania. Japo hakuweka wazi kipindi hicho kitarushwa hewani kupitia kituo cha habari cha shirika lipi.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments