Burudani

MC Pilipili aweka wazi jina la kitabu chake kipya

Mchekeshaji maarufu Emmanuel ‘MC Pilipili’ Mathias ametaja jina la kitabu chake kitakachozungumzia maisha yake.

15337141_211639752615297_415497833454501888_n

MC Pilipili amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM kuwa kitabu hicho kimegusa sehemu kubwa tatu ikiwemo kutoa burudani, elimu pamoja na tiba ya kisaikolojia.

“Namshukuru Mungu bado hakijakamilika lakini kimefika kurasa zaidi ya 100 sasa hivi. Kila kurasa utafafanua vizuri kabisa kwanini kimeitwa ‘Mtoto wa Nuru’. Mambo matatu makuu tuliyogusa ni pamoja na burudani, elimu na tiba ya kisaikolojia,” amesema.

Mchekeshaji huyo ameongeza kuwa kitabu hiko kimeandikwa na mwandishi maarufu Salum Kim Milongo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents