Bongo Movie

Mboto kutoa somo kwa makomedi

mboto

Msanii wa filamu na maigizo nchini anayezidi kushika kasi katika tasnia ya vichekesho, Mboto amedokeza kile anachokifikiria juu ya tasnia hiyo kwa mwaka wa 2011.

Akiongea na Bongo5 alisema lengo lake ni kushawishi wasanii wanaofanya vichekesho vya kujidhalilisha kwa kuvaa matambara waache na hatmaye wairudie sanaa kwa usafi na ustaarabu.

 

Aidha alisema watazamani wa sasa sio wale wa mwaka 47, wa sasa wapo kisasa zaidi na kutaka kuona mtiririko mzima wa matokeo na sio vipande vya maongezi ya kuchekesha.

“Nataka kufanya mabadiliko kwenye tasnia ya vichekesho, kwa kufanya ‘Series’ ya matukio na sio vipande vya maongezi kama ilivyokuwa zamani” alisema Mboto.

Haata hivyo msanii huyo alisema anataka kushawishi watanzania kuangalia vichekesho ‘Komedi’ kwani vinakuwa vinaleta ujumbe nzuru na sio mapenzi peke yake kama ilivyo filamu za kawaida.

Mboto pia alitolea mfano baadhi ya wasanii wakubwa nawao wameanza kubadilika na kufanya filamu za vichekesho, jambo ambalo linampa moyo kwamba wapo wengi watabadilika.

Huyu ndiye Mboto aliyetamba katika wimbo wa Sajna ‘Iveta’ na baadaye kuwa na soko kubwa kwa kutakiwa na wasanii wengi kushiriki katika filamu zao.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents