Burudani

Mbilia Bel aadhimisha miaka 40 ya uwepo wake kwenye muziki, aahidi kuachia albamu ya mwisho

Mbali na kusheherekea kuzaliwa kwa kutimiza miaka 57, mwanamuziki huyo Mboyo Moseka, aliyevuma kwa jina la ‘Mbilia Bel’ na kukonga nyoyo za watu wengi ameadhimisha pia miaka 40 ya kuweko kwake katika tasnia ya muziki.

Album yake mpya ya kuwaaga wapenzi wa muziki wake inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA Saleh Mwanamilongo amesema kustaafu kwake mwanamke huyu mashuhuri kutoka kwenye tasnia ya muziki, kumekuja mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa taarifa kwamba amefariki.

Akiongea Voa Swahili, Mbilia Bel amesema kwamba ataendelea kuwa mshauri wa wasichana chipukizi wanawania kuingia katika tasnia ya muziki hivi sasa.

Mwanamuziki Mbilia Bel, alipata sifa kubwa katika miaka ya 70 na thamanini kutokana na sauti yake nyororo.

Lakini hasa baada ya kujiunga na mwanamuziki TabuLey Rochereau. Pamoja na Tabu Ley, supasta huyu alipata umaarufu baada ya kuimba nyimbo nyingi zilitotungwa na Rochereau.

Hivi sasa Mbilia Bel amemaliza kurikodi album mpya ambayo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.

Album hiyo mpya anayoita “Signature” au saini ina nyimbo 21.

Katika ukanda wa Afrika mashariki Mbilia Bel ataendelea kumbukwa hasa kutokana na wimbo unaoitwa Nairobi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents