Habari

Mb Dog arudi kwa kishindo, aachia ngoma mpya na kufungua studio


Baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki, hatimaye Mb Dog amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘The Only One’ alioufanya kwenye studio yake mwenyewe aliyoifungua hivi karibuni, Makopa Inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao ‘Latifa’ amesema kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi kwenye game.
Katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Bongo5, Mb Dog amesema hana wasiwasi kuwa ataishika tena mioyo ya wapenzi wa muziki wa Tannzania kwakuwa haoni kipingamizi na muziki haujabadilika sana.
“Navyoona najua muziki umechangamka katika njia zake, lakini sio kwamba watu wamebadilika kuimba na muziki utafanyika vile vile kama watu walivyozoea kuusikia, sema tu katika kuanzia kuna harakati zitakuwa tofauti muda mfupi wakati nikitulia kwasababu muda mrefu nilikuwa sijajihusisha na haya mazoezi kwasababu ya mambo yangu binafsi,” alisema.
Aliongeza kuwa ujio wake mpya unaweza kuwa zaidi ya Latifa, “hilo ni miongoni mwa mawazo niliyonayo kwasababu sijaona kama kuna vitu tofauti vinavyofanyika labda vya chinichini ambavyo sivifahamu, lakini kimuziki tu naona uko kawaida na ntafanya vizuri zaidi ya hata hivyo.”
Mb Dog amesema hajamsahau P-Funk Majani ambaye ndiye alimtambulisha kwenye muziki wa Tanzania kwa kumtengenezea hit ya Latifa. “Ujue yeye ndo kama father kwenye muziki huu, ni mtu ambaye akinifanyia kazi anatumia nguvu nyingi sana lakini sasa nimerudi, nimefanya hii ngoma mwenyewe sasabu yeye pia ana kazi nyingi, lakini kwasababu muda upo lazima niende pale kupiga ngoma mbili tatu watu waziskie kutoka pale. Katika albam yangu kuna watu muhimu kama yeye hawawezi kukosa kunipigia nyimbo.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents