Burudani

Mazingira yalivyoshindwa kumbadilisha Ben Pol

King of Rnb Bongo, Benald Paulo maarufu kama Ben Pol ni mmoja kati ya wasanii wenye maisha ya kawaida yasiyokuwa na kiki za mitandaoni na mwenye respect inayomfanya tangu aanze muziki mpaka sasa ameonekana kuwa ni msanii wa pekee kuliko wote.

13129947_1620670814901499_611261908_n

Miaka sita iliyopita industry ya muziki bongo ilifanikiwa kumtambulisha Ben Pol kwa wimbo wake ‘Nikikupata.’ Hakika ni kipaji cha ukweli kilichotambulishwa kwa wakati huo hadi kumfanya kupata tuzo ya KTMA kama msanii bora chipukizi mwaka 2011.

Wanasema mazingira hubadilisha tabia, lakini imekuwa tofauti kwa Ben Pol. Msanii huyu hajabadilika kutokana na mazingira ya muziki na bado amezidi kukomaa kimuziki na kukua kiakili huku akiziacha mbwembwe na sifa zote kwa wasanii wenye vipaji hivyo.

Ben Pol amefanikiwa kutengeneza fan base yake inayozidi kuwa kubwa kutokana na muziki anaoimba kuweza kusikilizwa na kuaangaliwa na watu wa rika zote, kwenye hilo kiukweli hajawahi kuaribu.

Kumbuka wimbo wa ‘Sofia’ ulikuwa ni kama wimbo wa taifa na hata ukisikiliza wimbo wake mpya ‘Moyo Mashine’ ambapo hata ukiangalia video ya wimbo huo ngoma za masikio yako hazitachoka zaidi ya kupenda kuusikiliza na kuuona muda wote.

Hakika ameweza kuonesha kuwa kizuri hakijifichi kitaonekana kutokana na ubora ulionao pamoja na uzuri wake bila hata ya matangazo. Sijawahi kumuona Ben Pol akiwa amevaa hereni, kutoboa pua wala kuvaa vitu ambavyo vinatakiwa kutumika na watu wenye muonekano wa jinsia tofauti.

Alipohojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360, kinachoruka kupitia Clouds TV, alisema “najiogopa, nawaza hivi itakuwaje nikivaa hereni au kuchora matatoo. Wazazi hawatasumbua, kwa umri wangu huu naweza kufanya kitu chochote. Lakini mimi mwenyewe naona hivi itakuwaje, labda naenda kama benki hivi. Nataka kufocus kwenye muziki mzuri na ubunifu kwenye muziki lakini zile mbwembwe hapana.”

Hongera kwa msimamo wako Ben Pol wenye tija na manufaa kwa jamii ukiwa kama kioo cha jamii pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents