Bongo5 Makala

Maya Mia: Makeup artist maarufu duniani aishiye Tanzania, ana followers 1.5m Instagram, Youtube 810k (Picha/Video)

Sikumbuki ni lini nimeliona jina la Maya Mia kwenye Instagram na kuamua kumfollow ila ninachokumbuka ni kuona picha za msichana wa kizungu mwenye makeup zinazovutia sana na kuamua kumfollow bila kufahamu anaishi nchi gani.

10727519_1374856726163187_57666888_n
Maya Mia

Siku moja nakumbuka nilikuwa natafuta picha za Zanzibar kwenye Instagram na hivyo niliandika hashtag #Zanzibar na nikapata picha zote zilizopigwa Zanzibar na moja ikawa ya Maya Mia ambaye tayari nilikuwa namfollow kwenye Instagram.

10251448_1464141573868329_1075633811_n

Mara ya kwanza nilidhani kuwa pengine msanii huyu wa urembo alikuwa ameamua kwenda Zanzibar kama watalii wengine – sikuwa sahihi. Kumbe, Maya Mia, 32, ni mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania. Na nilijua hilo baada ya kuona picha yake nyingine kwenye Instagram ambayo kwenye sehemu ya location iliandika ‘Mbezi Beach, Dar es Salaam.’

Nilishangaa sana hasa baada ya kubaini kuwa kwa sasa ana followers zaidi ya milioni 1.5 kwenye Instagram na hivyo kumfanya awe mtu anayeishi Tanzania mwenye followers wengi zaidi katika mtandao huo mbele ya Diamond Platnumz mwenye followers zaidi ya laki nane sasa.

Maya Mia ni nani?

11377491_1029763237048806_863933114_n

Maya Mia ni makeup artist wa kimataifa raia wa Macedonia anayeishi jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alihamia jijini Dar miaka 10 iliyopita baada ya kuolewa na mtanzania anayeishi Dar.

Alizaliwa nchini Macedonia na kukulia huko huko. Baada ya kuolewa na kuhamia Tanzania ilimbidi ajifunze Kiswahili ambacho kwa sasa anakiongea bila wasiwasi – I mean anaweza kuongea kama watanzania wengine.

Wazazi wake ni watu wanaopenda sanaa na kutokana na kukua kwenye mazingira hayo alijikuta naye akipenda sanaa hasa ya uchoraji. Akiwa mdogo aliwahi kuwa model pia na alivutiwa sana na uwezo wa make-up artists katika kutumia mikono yao kubadilisha sura ya mwanamke na kumfanya avutie.

11184523_1572277996358461_1828630789_n

“Nilijua mara moja kuwa hiki ndicho ninataka kufanya,” anasema Maya kwenye video ya Youtube aliyoiweka kuelezea safari yake katika fani hiyo.

“Ninataka kuwabadilisha wanawake, nataka kufanya waonekane na wajisikie warembo. Sawa urembo huanzia ndani lakini unapovutia, unajisikia vizuri pia. Hivyo nilijua tu ntakuja kuwa make-up artist.”
Alianza kujifunza kutoka kwao na kujifunza pia yeye mwenyewe. Baada ya hapo watu walianza kumtafuta kutaka huduma yake japo awali hakuwa anatoza chochote. Baaada ya wateja kuwa wengi ndipo alipoanza kutoza gharama.

11357383_1452236168408871_1783213077_n

Alipokuja Tanzania mwaka 2004 na kufungua duka lake la nguo Maya Vintage Boutique pamoja na studio ya makeup, aligundua kuwa hakukuwa na make-up artists kabisa.

https://www.youtube.com/watch?v=8NfKrYodGnU

“Naamini nilikuwa mwenyewe tu kipindi hicho kwakuwa sikuwahi kumsikia au kukutana na yeyote aliyekuwa akifanya makeup, kwahiyo watu walikuwa wakisita kidogo kuhusu kwanini mtu anahitaji kufanyiwa makeup. Nilipoandikwa kwenye magazeti ya majarida ya ndani habari kuhusu mimi zilisambaa na watu wakazijua kazi zangu kwahiyo nikaanza kutafutwa na baadhi ya mastaa wa Tanzania walionitaka niwafanyie makeup kwa kava zao za album na magazine covers na photoshoot,” alisema Maya.

“Leo naweza kusema kuwa kuna make-up artists wengi nchini Tanzania na mapenzi kwa makeup yamekua na kiwanda kimepanuka hivyo nina furaha kuwa hapa kwenye wakati ambao kilikuwa kinapanuka na kukua.”

Lady Jaydee na Vanessa Mdee ni miongoni mwa mastaa waliowahi kufanyiwa makeup na Maya Mia.

11375799_859940754051879_1585616331_n

Hata hivyo kabla ya hapo alikuwa haoni haja ya kujiunga kwenye mitandao ya kijamii hadi pale rafiki zake walipomshawishi.
“Miaka kadhaa iliyopita rafiki yangu alinilazimisha nijiunge na Instagram,” anasema.

“Sikuwa napenda mitandao ya kijamii kwahiyo sikupenda kufungua akaunti hiyo lakini baada ya kushawishiwa sana niliamua kuifungua na nikawafollow makeup artists kadhaa waliokuwa wakionesha kazi zao na picha nzuri, hivyo niliamua kupost zangu mwenyewe, nilivutiwa sana. Nilipoanza kupost zangu watu wengi wakaanza kunifuata, kulike picha zangu na pia kuchangia na kuniomba kuweka picha tofauti na kuniomba kufungua akaunti ya Youtube ndio maana nina channel yangu leo.” Channel ya Youtube ya Maya ina watu zaidi ya laki nane hadi sasa.

Anasema kadri followers wake walivyoendelea kuwa wengi kwenye Instagram na Youtube, alijikuta akitafutwa na makampuni mengi ya bidhaa za makeup ambayo yalimtumia make-up zao kuzifanyia review na hiyo ikawa faida kwake sababu Tanzania haikuwa na maduka makubwa ya vipodozi.

Leo hii Maya amekuwa miongoni mwa makeup artists maarufu duniani na wanawake wengi wanaopenda kuvutia wamekuwa wakifuatilia tutorial zake kwenye channel yake ya Youtube.

Maya anatoa funzo ya jinsi mitandao ya kijamii inaweza kumfikisha mbali msanii.

“Amefanya kazi kubwa na sio ndogo kwenye industry ya makeup na yote ilianzia social media,” anasema Vanessa Mdee.

11429734_1617855375098303_1942322158_n

“Taratibu akaanza kuonekana na kufahamika kimataifa zaidi mpaka kutengeneza product zake.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents