Siasa

Maximo aongeza mwaka

Image
Marcio Maximo amekubali na kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja zaidi wa kuinoa timu yetu ya Taifa Stars.


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga alisema jana kuwa alikuwa na mazungumzo na Maximo na alikubali kuingia mkataba wa mwaka mmoja zaidi baada ya ule wa awali unaomalizika Julai mwaka huu.

Tenga alisema kuwa kuwa kilichowavuta hata kuongeza mkataba na kocha huyo ni kutokana na kuonyesha kiwango cha timu hiyo tangu alipoichukua miaka mitatu iliyopita.

Baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakitaka TFF kusaka kocha mwingine kutoka nchi kama Ufaransa, Jamhuri ya Czech, Serbia, Ubelgiji ambao viwango vinaonekana kuwa vya juu.

“Lengo letu sisi TFF na Tanzania kwa jumla tangu mwanzo tulikuwa tunataka tukae na Maximo kwa miaka minne na tulikuwa tunaamini kwa muda huo atakuwa ametusaidia kuiweka timu yetu katika hali nzuri na mafanikio makubwa” alisema Tenga.

Alisema kwa zaidi ya miaka 29 iliyopita kwa mara ya kwanza timu hiyo haijawahi kucheza fainali zozote na kocha huyo kwa mwaka huu katupeleka huko.

Rais huyo alisema pia Maximo katika kipindi chake chote hicho, Stars imecheza mechi 47, imeshinda mechi 21 sare 14 kufungwa 12 na hiyo siyo hatua ndogo ukizingatia timu ya Taifa Stars bado changa.

Aliwashukuru wadau wote wa michezo walioifikisha timu hiyo hapo ilipo akiwemo Rais Jakaya Kikwete, mawaziri,wabunge na kuahidi kutafuta wadhamini zaidi.

Rais huyo wa TFF alisema matumaini ya watu wengi saidi ni kuona Stars safari ijayo inacheza fainali za CHAN mwaka 2011 nchini Sudan na mwaka 2014 inashiriki Kombe la Dunia zitakazochezwa Brazil.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents