Burudani

Maua Sama awataja waandishi wa ngoma yake mpya ya Main Chick

Siku hizi limekuwa ni jambo la kawaida kwa wasanii wetu wa Bongo kuandikiana nyimbo,lakini linapokuja suala la kuwapa credits waandishi hapo ndio wengi hupata Kigugumizi kuwaweka wazi.

Suala la kigugumizi halikuwepo kwa Maua Sama alipokuwa akihojiwa na Prince Ramalove Kupitia Kings Fm,kwani aliwaweka wazi waandishi wa ngoma yake inayofanya vizuri kwa sasa,Main Chick.

“Wakati nafanya kuandika nyimbo,nilikuwa niko na Don Flavour pamoja na Ibra Nation,kwahiyo idea ya Main Chick ilitokea Pale,” amesema Maua.

“Hawa wawili wametumia nafasi kubwa sana katika kufanya wimbo wangu umekuwa mzuri,kimsingi wao ndio waandishi wa wimbo.”

Kwa asiyefahamu, Don Maswaga ndiye aliyeandika pia One Day ya Nandy na ngoma nyingine za Maua ambazo Bado hazijatoka, na Ibra Nation anafanya vizuri na Sukari Guru ambayo amempa shavu Maua Sama Pia.

By Prince Ramalove
Kings Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents