Burudani

Maua Sama adai siku FA amempigia simu kumwambia amependa uimbaji wake alidhani ‘changa la macho’

Maua Sama, enzi hizo hajulikani kabisa kimuziki, alipokea simu kutoka kwa Mwana FA, mtu aliyekuwa akimsikia tu au kumwona kwenye TV akimsifia kwa uimbaji wake mahiri. Ilikuwa ni simu iliyomshtua muimbaji huyo na kudhani kuwa anataka kuingizwa mjini na wajanja.

“Sikuamini,” Maua alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.

“Kwanza niliona si unajua wale watu wa mtandao mtandao wanataka kuzingua kwahiyo kwangu mimi nikaona kabisa.. kwanza kanipigia simu ananiuliza ‘unajua unaongea na nani’ nikamuambia hapana ‘Mwana FA, Hamis’, nikamuambia ‘Hamis? Hamis gani?’ akaniambia ‘Hamis Mwinjuma’ nikamuambia mimi simjui mimi nilikuwa najua tu Mwana FA. So he told me ‘Mimi ni Mwana FA msanii, nimesikia ngoma zako nimetumiwa na your sister I wanna hear the song and stuff.’Nikamuambia ‘mhh,”amesimulia.

“Imagine uko Moshi somewhere kwenye kochi umekaa you have some stress about school kesho asubuhi una vipindi and out of nowhere Mwana FA anakupigia. I was like ‘hey this is a joke don’t play with me.’

Baada ya FA kujieleza vya kutosha ndipo Maua alipoamini kweli na kuamua kutoroka, kupanda basi kuja Dar na wimbo wake wa kwanza So Crazy aliomshirikisha FA ulipotoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents