Burudani

Mchekeshaji Mau adai kuanza kuona mwanga

Msanii wa komedi Maulid Ali maarufu kama Maufundi amesema kwa sasa amekuwa akipata pesa kutumia mitandao ya kijamii zaidi kwa kufanya video za muziki za vichekesho, parody.

MAU

Akiongea na Bongo5, Mau alisema kuwa kwa sasa amepata style mpya ya kumuingizia pesa ambayo mara ya kwanza alikuwa anafanya kama burudani lakini amegundua kuwa kupitia hivyo pia anaweza kuvuta mkwanja.

“Unajua mwanzo nilikuwa nafanya kama kujifurahisha lakini sasa hivi nimeona hii ni fursa na nimekuwa nikipata simu nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali na imekuwa ikiniingizia pesa,” amesema. “Kwa sasa kuna wasanii wananilipa na pia napata pesa kupitia Youtube. Kwa upande wa malipo kwakweli wasanii wachanga ndio wanalipa vizuri zaidi na mimi natafuta pesa ndugu yangu na bado napokea maombi mengi na zipo nyingine zinakuja nashukuru kwa watu kunielewa nachofanya,” ameongeza.

Hadi sasa Mau ameshafanya parody za nyimbo kadhaa ikiwemo Jike Shupa ya Nuh Mziwanda na Kwetu ya Raymond. Ukitaka kuona video hizi ingia www.vichekotime.com.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents