Habari

Matukio ya kumwagiwa tindikali yamwogopesha Mange Kimambi kurudi Bongo, apanga kuja na ‘acid cover’

Matukio mabaya ya kumwagiwa tindikali ambayo yameibuka nchini yamemtia mashaka mwanamitindo na mbunifu wa mavazi, Mange Kimambi anayeishi na kufanyia shughuli zake nje ya Tanzania. Hata hivyo amesema akija atakuwa amechukua tahadhari, acid cover.

kkkk

Amesema atakaporejea Tanzania atavaa kava maalum usoni ili na yeye asije akamwagiwa.

“Duh Bongo pamechafuka aiseeee….. … Inatisha sana…. Yaani lazima nipige hiki kitu nikiwa Bongo….nsije pofuliwa macho bure…..hehhhehe,” aliandika kwenye Instagram.

“Hivi huyu aliyemwagia alijuaje kuwa atamkuta outside his supermarket at that particular moment and at that particular supermarket?…Duh, i smell conspiracy …Aisee nikija bongo ntajiweka tindikali cover.”

Hivi karibuni mmiliki wa Home Shopping Centre alimwagiwa tindikali usoni na hadi sasa amelazwa nje ya nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents