Burudani

Master J aeleza kwanini haiwezekani maproducer wa Bongo kufanikiwa kama wasanii na kwanini alistaafu

Producer mkongwe wa muziki nchini na CEO wa MJ Records, Master J, amesema ni ndoto kwa watayarishaji wa muziki nchini kufanikiwa kama ilivyo kwa wasanii wanaowatengenezea nyimbo.

Master Jay akibadilishana mawazo na mdau

Akiongea na Bongo5, Master J amesema hilo ndilo lililomfanya aache kutengeneza muziki na kuingia kwenye biashara zaidi. Amesema sababu kubwa iliyotengeneza hali hiyo ni maproducer wa Tanzania kutokuwa na umoja ambao ungewafanya kuwa na msimamo unaofanana, bei sawa za kurekodia na utaratibu ambao ungewezesha wanufainike na matumizi ya nyimbo wanazotayarisha.

Ameeleza kuwa mara nyingi uhusiano kati ya producer na msanii huharibika pale ambapo wimbo unapomuingizia fedha nyingi msanii kupitia show, matangazo ama ringtone wakati aliyeutengeneza akiendelea kuwa na maisha magumu.

“Unakubali pale mwanzoni lakini mwisho wa siku unakuja kugundua producer nimenyanyuliwa na mtu kama Diamond mpaka hapa sasa najulikana na sifa zote lakini huna gari, huna uwezo wa kuvaa nguo nzuri, huna hela ya kuishi sehemu nzuri, kwahiyo mwisho wa siku unakuwa mtu wa kuchekwa tu. Ndio hapo producer roho huanza kumuuma anaanza kugombana na msanii,” amesema Jay.

“Ndio maana hata mimi nikastaafu, mimi mwisho wa siku nilikuwa nataka watoto wangu wasome kwenye shule fulani, waende kwenye university fulani, nikaona hicho kitu nikaona nikiendelea hivi sitaweza kufanikisha hayo kwa kupitia muziki. Ndio maana nikachukua hela yangu ile Mungu alinijalia kwenye muziki nikawekeza kwenye biashara nyingine, bahati nzuri namshukuru mwenyezi Mungu alinipa akili ya kufanya biashara.”

Master Jay
Watoto wa Master J

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents