Burudani

Mastaa wa BSS 2012 kuburudisha Dodoma Ijumaa hii

bss

Washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search wanatarajia kuanza ziara za mikoani ambapo wataanzia mjini Dodoma Ijumaa hii kwenye ukumbi wa Maisha Club ikifuatiwa na Dar es Salaam.

Ziara hiyo itajumuisha vijana walioingia kumi bora, akiwamo Menina Atick, Nsami Nkwabi, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chilambo.

Katika ziara hiyo pia, ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2006, wapenzi wa muziki watapata fursa ya kumshuhudia mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo ambaye atakuwa akizundua wimbo wake siku hiyo.

Kwa upande wake mshindi wa Epiq BSS, Walter Chilambo alisema mashabiki watarajie burudani kali kutoka kwake. “Nimejipanga sana kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania kuwa hawakukokosea kunipigia kura niwe mshindi’ alisema Walter jana wakati washiriki hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.

Wasanii wengine watakaotoa burudani kwenye ziara hii ni Barnaba, Ben Paul, Linah na Ali Nipishe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents