Burudani

Masoud Masoud: ‘Siwezi kumlinganisha Diamond na Ali Kiba’ adai Alikiba angekuwa nje asingekamatika

Wiki iliyopita katika kipindi cha Mkasi ambacho hurushwa kupitia EATV na kuendeshwa na mtangazaji Salama Jabir, mgeni alikuwa Masoud Masoud, mtangazaji mahiri wa muda mrefu ambaye ni miongoni mwa watangazaji wa Radio wanaoheshimika sana Tanzania kutokana na upeo mkubwa alionao na kufahamu mambo mengi.

Masoud
Masoud

Moja ya swali aliloulizwa ni “Labda kuna tamasha wewe ndio muandaaji au wamekwambia uchague mwanamuziki ambaye ataenda kuburudisha kwenye hilo tamasha Tanzania utamchagua mwanamuziki gani?”

Masoud ambaye anasifa ya kuongea kwa uwazi bila kupindisha maneno alimtaja Alikiba kuwa ndiye msanii pekee wa bongo fleva anayemkubali kuliko mwingine yeyote.

Alikiba2
Alikiba

“Mimi wa kwanza nitakayempendekeza aaah nani huyu, nampenda sana katika wasanii wote wa bongo fleva, Alikiba, Alikiba nampenda sana. Alikiba kama umemsikiliza, Rhyme zake zile katikati ya zile bars anavyoimba ni mwanamuziki kama angekuwa nje ya nchi asingekamatika. Angepata producer mzuri wa kumfahamisha nini cha kuimba beat gani atumie, Alikiba yuko juu sana.” Alijibu Masoud

diamond3
Diamond

Aliendelea na kuongeza kuwa Diamond anaweza kuwa anafanya vizuri sokoni lakini hawezi kumfikia hata kidogo Kiba katika uimbaji.

“Nyota imeng’aa kwa Diamond Platnumz lakini Diamond Platnumz siwezi kumlinganisha hata kidogo na Alikiba, kwenye kuuza huwezi kumlaumu anaweza kuwa Diamond akauza sana au akampandisha na si Tanzania tu, hata Hollywood wanafanya hivyo hata CBS wanafanya hivyo, hata US music industry wanfanya hivyo. Sasa mpaka wakiwepo watu wataalam wanaoweza kusema huyu anaimba sawa huyu haimbi sawa lakini kwenye mauzo hakuna mtu anajali hilo.”

Masoud kwa sasa ni mtangazaji wa TBC Taifa.

Mtazame hapa kupitia Mkasi (sogeza hadi dakika 17:45 alipozungumzia kuhusu Alikiba na Diamond)

Source: MkasiTV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents