Michezo
Mashabiki wa Chelsea wamzomea Hazard
Baada ya Chelsea kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na timu ya PSG kwa jumla ya magoli 4-2, Hazard ameingia kwenye mzozo na mashabiki wa timu hiyo baada ya kubadilishana jezi na Di Maria.
Hazard alijikuta akizomewa na mashabiki wa timu yake ya Chelsea baada ya kubadilishana jezi na Di Maria kipindi cha mapumziko wakati huo timu hizo zikiwa zimefungana goli moja kwa moja, kipindi cha pili Ibrahimovic aliifungia PSG goli la pili na la ushindi.
Kocha wa Chelsea, Guus Hiddink amesema,”Ndio, walikuwa sahihi kufanya walichokuwa wanakifikiria. Siyo mbaya kuonyesha hisia zako.”