Burudani

Mase aachana na uchungaji kimoja, sasa kufanya muziki ‘full time’

Baada ya kumtumikia Mungu kwa muda mrefu kama mchungaji, rapper wa zamani wa Bad Boy, Mase ambaye aliuweka kando muziki toka mwaka 1999, ameamua kuachana na uchungaji na kurejea kwenye maisha yake ya zamani ili afanye muziki kikamilifu.

Kwa mujibu wa ripoti, Mase ameachana kimoja na kanisa lake la El Elyon International, na sasa ataanza kutumbuiza kwenye matamasha mbalimbali ya Hip Hop kama ilivyokuwa zamani.

“I feel like I never really left. I did a lot of music behind the scenes working with people. So the music that is out right now, I have a lot of input in it.” Alisema Mase.

Hivi karibuni wakati wa tuzo za BET, Mase aliuambia mtandao wa Hip Hop Hollywood kuwa single yake inayokuja inaitwa ‘Billboard’, ambayo amewashirikisha Rick Ross na Kanye West.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents