Habari

Marufuku nyaraka za ofisi kuhamishiwa nyumbani – DC Hapi

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi amepiga marufuku viongozi wa mitaa kuhamishia nyaraka za serikali katika nyumba zao binafsi kwa kuwa ni kinyume cha sheria na watakaokaidi agizo hilo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Ametoa agizo kwa wenyeviti na watendaji wa mitaa na kata ya wilaya hiyo, baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa mgogoro kuwa katika Mtaa wa Malindi, Kata ya Mbweni uliosababisha kuwepo kwa ofisi mbili moja, ikiwa ni ya serikali na nyingine ikiwa nyumbani kwa Bariki Elibariki ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa huo.

Hapi alisema, “Hili suala la ofisi ya serikali kuwa nyumbani kwa mtu binafsi haikubaliki hata kidogo na kuna waraka uliotolewa na mkurugenzi kupiga marufuku suala hilo. Nyaraka za serikali haziwezi kukaa kwa mtu binafsi labda kama hiyo ni ofisi yako na mkeo, hilo halituhusu.”

Aidha DC Hapi alimtaka mwenyekiti huyo na Mtendaji wa Mtaa huo, Abdallah Mkeyenge kukaa chini na kumaliza tofauti zao ambazo kwa sasa zimefikia katika hatua mbaya ya kutoleana lugha za vitisho na kudhalilishana hadharani.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents