Burudani

Marco Chali: Enrico, P-Funk na Master J wameupigania muziki wa kizazi kipya Tanzania

Producer Marco Chali wa MJ Records, amewataja watayarishaji wakongwe wa muziki nchini, Enrico, P-Funk na Master J kuwa ndio walioupigia muziki wa kizazi kipya.

1517242_434330776709684_1387853801_n

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Marco aliwataja watayarishaji hao kama watu anaowakubali zaidi na waliojitolea kuukuza muziki wa Bongo Flava.

“Ni jamaa ambao kwanza wamefight sana huu muziki wa Bongo Flava kwa kuanza walikoanzia unaona wameenda halafu ukiangalia utaona sio kwamba walikuwa wanafanya kazi sababu wanataka sana hela, walikuwa wameanza hii kazi sababu ni kitu ambacho kipo kwenye mioyo yao,” alisema Marco.

“Ndio maana unakuta mtu kama Master J kitu alichokisomea na kazi anayofanya ni vitu viwili tofauti. Kwahiyo mwisho wa siku unakuja kugundua kuwa ni watu ambao wameuanzisha muziki sio kwasababu ya hela tu au kwasababu wameona sanaa inalipa au nini, wameanzisha kutoka moyoni. Na ndio maana mpaka sasa hivi unaona wao ndio wanarun hii game. Na ukiangalia vitu vingi, wasanii wengi waliotoka wametoka kwenye mikono ya hawa watu,” aliongeza Chali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents