Habari

Maoni: Millard Ayo ndiye mtangazaji wa vipindi vya burudani aliyeng’ara zaidi mwaka 2012

ayo (600x450)

Si jambo la kushangaza kwa wengi kuhusu umaarufu wa mtangazaji huyu kijana nchini. Ndiye mtangazaji mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao wa Twitter kuzidi mtangazaji yeyote (followers 28,872) na pia ndiye mtangazaji mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mtandao wa Facebook kuliko mwingine yeyote nchini (likes 60,066).

Ni mtangazaji wa kipindi maarufu cha Amplifaya cha Clouds FM. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Bongo5 kupitia Facebook, Millard ndiye aliyetajwa na watu wengi zaidi kama mtangazaji bora wa vipindi vya burudani mwaka 2012.

Nafasi ya pili imekamatwa na Adam Mchomvu akifuatiwa na B12 wote wa Clouds FM. Wengine waliotajwa zaidi ni Dj Fetty wa Clouds FM, Sam Misago na Abdallah Ambua wa East Africa TV.

Hongera kwa wote waliofanya vizuri na endeeleni kukaza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents