Burudani
Mansu-Li arudi shule kusomea fani ya manunuzi
Rapper wa kundi la Capitol Letters, Mansu-Li amerudi shule kusomea fani ya manunuzi ijulikanayo kama ‘Procurement and Logistics katika chuo cha Tanzania cha mahesabu, TAA, mkoani Mtwara.
Akiongea na kipindi cha New Chapter cha Radio Free Africa, hivi karibuni, rapper huyo alidai kuwa ameamua kurudi shule ili kujihakikisha mustakabali mzuri wa maisha yake kwakuwa muziki hauleweki.
Amesema kozi anayosoma itamchukua kipindi cha miaka miwili kumaliza.
“Ni course ya Diploma, sababu ni vitu ambavyo sijawahi kuvisomea nikaona ni fresh nikianza na Diploma,” amesema Mansu-Li.