Michezo

Manny Pacquiao na Amir Khan kupambana April mwaka huu

Manny Pacquiao na Amir Khan watapambana April 23 ya mwaka huu ulingoni.

Mabondia hao wote wawili wamethibitisha kushiriki kwenye pambano hilo. Kupitia mtandao wa Twitter Pacquiao ameandika, “Negotiations between team Pacquiao and team Khan have come to terms for the April 23 bout as this is what the fans wanted. #PacquiaoKhan.”

Naye Khan kupitia mtandao huo ameandika, “It’s OFFICIAL our founder @amirkingkhan will fight @mannypacquiao on April 23 we wish Amir the very best #SuperFight.”

Japo mpaka sasa haijajulikana ni sehemu gani pambano hilo litafanyika lakini kwa mujibu wa Khan amedai kuwa pambano hilo linaweza kufanyika Uingereza, Dubai au Marekani.

Pambano hilo limekuja baada ya wiki chache zilizopita Pacquiao kuwaorodhesha mabondia wanne akiwemo ilimashabiki wake wapige kura yupi apigane naye. Khan aliongoza kwa kupata kura 48%, Kell Brook 24%, Terence Crawford 21% na Jeff Horn 7%.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents