Michezo

Manchester United yatinga fainali ya EFL

Klabu ya Soka ya Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la EFL (Capital One) baada ya kuifunga Hull City jumla ya mabao 3-2 katika nusu fainali mbili za kombe hilo.

Katika nusu fainali ya pili iliyochezwa Alhamisi hii katika uwanja wa nyumbani wa Hull City wa Kingston Communications, timu hiyo ilifanikiwa kuifunga Man United kwa mabao 2-1 huku mabao ya timu hiyo yakifungwa na Tom Huddlestone dakika ya 35 na Oumar Niasse dakika ya 85 na goli na United lilifungwa na Paul Pogba dakika ya 66.

Aidha katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliofanyika Januari 10 ya mwaka huu United wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford walifanikiwa kushinda mabao 2-0 huku magoli yake yakifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini.

Sasa timu hiyo inatarajia kukutana na Southampton kwenye mchezo wa fainali utakaofanyika katika uwanja wa Wembley Jumapili ya Februari 26 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents