Habari

Manchester United yaichapa 4-1 Leicester Cty

Manchester United Jumamosi hii imerudisha furaha kwa mashabiki wake baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya mabingwa watetezi wa Premier League, Leicester Cty.
man-utd-10-1

United ambayo ilikuwa kwenye Uwanja wa nyumbani, Old Trafford ilionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika mabao yote manne huku nahodha wake, Rooney akianzia benchi.

Kwa matokeo haya, United inaongeza alama tatu na hivyo kufikisha jumla ya pointi 12 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo wamefanikiwa kushinda michezo minne, imepoteza miwili na haijatoa sare.

Mabao ya United leo yalifungwa na: Smalling dakika ya 22; Mata (36), Rashford (39), Pogba (42) huku lile la Leicester likiwekwa kimiani na Gray dakika ya 60.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents