Michezo

Manchester United: Tuna furaha kuwa na Louis van Gaal

Klabu ya Manchester United imedai ina furaha na kocha wao Louis van Gaal kama kocha wao, kwa mujibu wa vyanzo vya Sky Sport.

lvgee

Taarifa kutoka katika magazeti ya siku ya Alhamisi zinadai Jose Mourinho anajiandaa kupewa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Van Gaal kama kocha wa Manchester United kwa mshahara wa pauni milioni 15 kwa mwaka.

Imedaiwa Mourinho pia anataka kumleta kiongozi wa michezo wa Atletico Madrid, Andrea Berta.

Mustakabali wa Van Gaal umeingia katika sintofahamu katika majuma ya hivi karibuni, huku United ikiwa alama sita nyuma ya vinara na kuwafanya wawe katika nafasi ya kutofuza ligi ya mabingwa Ulaya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents