Burudani

Man Water kuja na ‘mobile studio’, studio ya kuzunguka mitaani kwenye gari ya ‘Ambulance’

Mshindi wa tuzo ya ‘Myarishaji Bora Wa Mwaka Kizazi Kipya’ KTMA 2014, Man Water wa Combination Sound amezungumzia mpango wake wa kuja na ‘mobile studio,’ yaani studio ya kwenye gari itakayokuwa ikizunguka mitaani kuwafata na kuwarekodi wateja wake popote pale walipo.

water

“Mobile studio kwa namna ya kusave cost, haitakuwa na gharama sana mi nadhani, ni kitu kwanza cha kipekee lakini pia kina uwezo wa kuwafikia wateja fasta zaidi” alisema Man Water kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Water ambaye ndiye producer wa single mpya ya Alikiba ‘Mwana’ amesema aina ya magari atakayotumia kufunga studio inayotembea (mobile studio), ni yale yanayotengenezwa maalum kwaajili ya kubeba wagonjwa (ambulance).

“Nitapunguza hizo gharama kwa magari ambayo yatanigharimu kwa kulinunua tu, lakini yatakuwa yako vizuri kwenye matumizi ya mafuta na vitu vingine kama hivyo, kwahiyo kwa haraka haraka ni magari yanaweza kuwa jamii ya ambulance, kwasababu ambulance iko sound proof imeshatengenezwa kabisa kwaajili ya wagonjwa kwahiyo haitoingiza kelele kwa kiasi kikubwa sana kama ingekuwa gari nyingine ambayo ingebidi niijenge sana katika kupata sound proof, ni mfumo kama van flani, ni OB Van kwa kifupi.”

Ameongeza kuwa mpango wake ulikuwa ni kupeleka studio hizo za kwenye gari mikoani, lakini kwa kuanzia ataanza kutoa huduma hiyo Dar.

“Target ilikuwa mikoani ila kwa kuanza tutapiga route za hapa hapa mjini kwa watu ambao wana deal na matangazo, labda tu nisiendelee kutoa idea sana kwasababu unajua watu wanaweza waka bite hii idea wakafanya, ila napenda kuiongea mara kwa mara ili watu pia wajue founder wa hii idea ni nani ili hata kama atatokea mtu ambaye amenitangulia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents