Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Man United yasonga nusu fainali Europa League, Samatta hoi njiani

By  | 

Usiku wa jana (Alhamisi) zilichezwa mechi nne katika viwanja tofauti kwenye kombe la ligi ya Europa. Timu ya Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo baada ya kufanikiwa kuifunga Anderlecht ua Ubelgiji kwa mabao 2-1 na kufanya kufuzu katika hatua hiyo kwa jumla ya magoli 3-2.

Nayo Ajax ya Uholanzi imefuzu katika hatua hiyo japo ilifungwa kwa mabao 3-2 na Schalke 04 ya Ujerumani, lakini katika matokeo ya Jumla yanaifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-3.

Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku huo klabu ya Olympique Lyonnais, imeungana na timu nyingine katika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Beşiktaş kwa njia ya mikwaju ya penalty ambao walishinda kwa 7-6. Katika dakika 120 za mchezo huo Beşiktaş ilishinda 2-1 na kufanya timu hizo kufungana jumla ya mabao 3-3, ambapo katika mchezo wa kwanza Lyon ilishinda kwa mabao 2-1.

Wakati huo huo timu ya KRC Genk anayoichezea Mbwana Samatta kutoka Tanzania, iliondolewa katika mashindano hayo na Celta de Vigo ya Hispania japo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Katika mchezo wa mwanzoni, Genk walifungwa mabao 3-2 na kufanya jumla ya matokeo yote kuwa 4-3.

Droo ya timu zitakazo kutana katika hatua hiyo ya nusu fainali inatarajiwa kupangwa leo.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW