Michezo

Man U wakubali kumuuza Morgan Schneiderlin Everton

By  | 

Klabu ya Manchester United na Everton wamekubaliana ada ya uhamisho wa Morgan Schneiderlin kijiunga na Everton, Everton imekubali kulipa paundi £22m na leo anategemewa kufanyiwa vipimo.

Mfaransa ambaye ana umri wa miaka, 27, alinunuliwa na Manchester United kwa kitita cha paundi milioni 25 kutoka Southampton mwezi Julai 2015 chini ya kocha Louis van Gaal.

Kufuatia ushindi wa Man U wa 2-0 dhidi ya Hull City, Morinho alisema: “naibu mwenyekti Ed Woodward ameniarifu kwamba mpango wa kumuuza unakaribia kukamilika”

Ameiwakilisha Man U mara 47, japo chini ya ukufunzi wa Jose Morinho msimu amecheza mara 8 pekee, mara tatu katika dimba la ligi kuu ya Uingereza.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments