Michezo

Man City huenda wakamkosa Gabriel Jesus msimu wote

Mshambuliaji wa klabu ya Man City Gabriel Jesus imeripotiwa kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobaki kufuatia kuumia katika mguu wake kwenye mechi ya jana dhidi ya Bournemouth ambayo City walishinda goli 2-0.

Jesus ambaye ametua City mwezi Januari akitokea Palmeiras kwa ada ya pauni milioni 27, ameonekana akiwa amavaa kiatu cha kujikinga (Protective Boot) huku akitembea kwa msaada wa magongo huko jijini Manchester.

Taarifa kutoka kwa klabu ya Man City inathibitisha kuwa Mbrazil huyo amevunjika mfupa (The Fifth Metatasar) katika mguu wake wa kulia na atapata vipimo zaidi siku zijazo ili kujua ni kwa muda gani atakaa nje.

Gabriel Jesus mpaka sasa ameichezea City mechi 5 akifunga jumla ya magoli matatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents