Burudani

Mambo ya kufanya unapotafuta mfanyabiashara mwenza

Kama wewe ni mjasiriamali inawezekana ukawa unatafuta mtu wa kufanya naye biashara au kufungua kampuni pamoja. Inawezekana unatafuta watu wenye vipaji na uzoefu ili ufanye nao biashara pamoja ili kukuza soko lako. Hayo tote yanaweza kuwa ya msingi akin unapotafunza mwenza kibiashara kuna mambo ya kuzingatia;

SA-image-business-woman-2

1. Fanya kwa umakini. kila mtu anavutia mnapokuwa kwenye hafla au shughuli yoyote ya kibiashara lakini unapokuwa unaingia mkataba wa kibiashara hakikisha unamshika mkono mtu sahihi. Mfuatilie huyo mtu kwa ukaribu usiishie tu kwa marafiki zake au rafiki zako, wasiliana na watu waliofanya nae biashara, wateja wake, na kwenye mitandao ya jamii. Unaweza kupata majibu ambayo yatakusaidia kuingia kwenye mkataba na huyo mtu.

2. Weka Nyaraka ya kila kitu kama unaona kuweka nyaraka ya kila kitu mnapoanza biashara si mambo la msingi basi unapotea kuanzia hapo. Unapoanza kufanya biashara na mtu mwingine hakikisha kila makubaliano yawe kwenye maandishi, malengo ya hiyo biashara, majukumu ya kila mmoja na namna ambayo unaweza kutoka kwenye makubaliano hayo.  Kila kifungu cha makubaliano hakikisha kimegongwa mhuri na wakili wako au wenu, na vile vile kwakuwa mtatakiwa kulipa kodi hakikisha mapato na matumizi yanahakikiwa na mhasibu.

3. Hakikisha una mpango wa kutokea Kuacha hiyo biashara ni kitu cha kwanza kufikiri wakati unaanzisha. Unatakiwa kuwa na mpango madhubuti wakati wa kuanzisha hiyo biashara na namna utakavyotoka. Pangilia kisheria namna ya kugawana mali za biashara na namna ambavyo mali zenu zitakavyofanya kama mmoja wenu atafariki.

4. Jilinde  Namna nyingine ambayo unatakiwa kuwa naYo ni kujilinda, hakikisha unalinda mali zako binafsi zisihusishwe na mali za kampuni.

5. Linda bidhaa au jina lako la bidhaa Kuunganisha biashara au mawazo kunahitaji kufanya kazi kubwa, kitu kingine unaweza kujikuta unapoteza mwelekeo. Usipoteze mwelekeo wa wewe ni mani na nina lako la bidhaa ulilojijengea. Kama mpango wenu ulikuwa utahakikisha bidhaa uliyonayo iendelee kuwa sokoni inabidi ufanye hivyo kuilinda isipotee.

Unapokutana na mtu ambaye atakuwa mfanyabiashara mwenza, wewe unaweza angalia malengo yako na namna gani yanashabihiana na ya mwenzako lakini kitu cha msingi ni mahusiano yenu yaws mazuri. Hakikisha mnafanya kazi kwa pamoja kwa lengo moja si kila mtu na malengo yake katika kampuni moja.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents