Habari

Mambo ya kufahamu pale unapoanzisha mahusiano na bosi wako

Sawa, una mahusiano na bosi wako. Nini kinafuata?  Je una mpango wa kuwa na mahusiano na bosi wako? Je ni mambo gani unatakiwa kujua?

Amini usiamini , mahusiano katika eneo la kazi  ni kawaida tu na inawezekana hauko peke yako. Mahusiano yanaathiri warembo, walioelimika na wasioelimika, matajiri na maskini kwenye makampuni madogo na makubwa sehemu zote. Kama umeingia au una mpango wa kuingia unaweka maisha yako ya kazini kuwa magumu na tata. Si mara zote watu hutoka na kudhamiria kuwa na mahusiano kazini ila hujikuta yametokea.

Affairs with your boss

Una mahusiano na bosi wako, kitu gani unapaswa kujua, kama haujaanza mahusiano jaribu kuangalia vitu hivi,

1. Je Kampuni unayofanya kazi ina sheria inayohusu mahusiano kazini? Kama ni ndio unajiwekea mazingira magumu na kuhatarisha kazi yako. Hata kama mtu unayeingia naye kwenye mahusiano ni bosi wako, wewe ndiye utakayeondoka . Mtu mwenye cheo mara zote anabaki kwenye kampuni, kampuni haiwezi kuingia gharama ya kumpoteza bosi kwaajili ya mahusiano yako, ila wewe itabidi uondolewe kwakuwa gharama ya kumpata bosi ni kubwa kuliko kupata mtu kama wewe.

2. Uliajiriwa kwa ujuzi wako na si vinginevyo, baada ya kuanza mahusiano mambo yanaanza kuwa tata kikazi. Bosi wako ni bosi wako tu, yeye ndiye anayeamua nani apandishwe cheo, kupata nyongeza za mishahara na mengine mengi. Hivyo mambo yataanza moto moto ila siku za usomi huanza kufifia na kinachobakia ni  kutojisikia vizuri unapokuwa kazini. Hivyo uwe makini na maamuzi unayoyafanya hasa kuhusu mahusiano kazini.

3. Kumbuka mahusiano hayo yatafika mwisho, utajisikiaje unakwenda ofisini na umeshaachana na bosi wako, utendaji wa kazi utakuwaje? Utakuwa na maumivu  makubwa, ingawa watu wengi hujifanya hawajaumia.

Kama Bosi wako ameoa au kuolewa ….…

1. Kumbuka asilimia kumi ya mahusiano kazini ndio yanaweza kwenda kwa muda mrefu.  Mahusiano mengi huishia kuvunjika na kuacha maumivu makubwa.

2. Je haya ni mahusiano yako ya kwanza? Je ni ya kwako? Kumbuka watu wana vitu vingi vinavyoendelea kwenye maisha yao na mahusiano, tabia na hulka tofauti hivyo uwe makini.

Kama unaamua kuingia kwenye mahusiano………..

1. Uwe makini na utumie akili nyingi, unamwambia nani hapo kazini, ili usiweke hatarini kazi yako au kazi inayokuja ndani ya kampuni hiyo hiyo kama kupandishwa cheo n.k

2. Kama umeoa au kuolewa wewe ni mdanganyifu kwenye ndoa yako, jaribu kujua na kutafutana kuongea na mwenzi wako kitu gani kinapungua kwenye ndoa yenu .Hiyo ndo namna ya kuonyesha upendo kwa mtu uliyeamua kuishi naye kwenye ndoa.

3. Jaribu kwenda kwa washauri wa mambo ya ndoa na mahusiano waweze kukusaidia. 

Uamuzi ni wa kwako, fikiria kwa makini na tafakari .

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents