Habari

Mambo 9 ambayo watu waliofanikiwa huyafanya

Unafahamu mambo ambayo watu waliofanikiwa hufanya ili kuendelea kutulia, kuridhika, kumiliki na kutawala mazingira yao? Kuna baadhi ya tabia ambazo huendelea kuzitumia na ambazo zimewaweza kuboresha utendaji wao ni kama vifuatavyo;

nr_ursulaburns_2007

1. Hawaruhusu mtu peyote kuzuia furaha yao 
Wakati wewe kuonekana una furaha lazima ujilinganishe na mtu mwingine bali watu waliofanikiwa wanamiliki furaha yao wenyewe bila kujali nani amewazunguka. Kwahiyo wanapopata mambo ya kuwafurahisha hufurahi bila kuruhusu mawazo ya watu wengine kuchambua furaha yao au la!

Ni vigumu kuzuia mawazo ya watu wengine au namna watu wanavyofikiri juu yako lakini hupaswi kujilinganisha na watu hao.Haijalishi watu wanawaza mini kuhusu wewe, wewe ni mtu kamili na wa tofauti kuliko mtu mwingine na una thamani ya kipekee kabisa kufurahia utu wako kwa hali coyote na katika mazingira yoyote.

2. Watu waliofanikiwa Hawasahau 
Watu wa namna hii ni rahisi kusamehe lakini haimaanishi wamesahau. Msamaha ni kurusu jambo ulilotendewa lipite na uendelee na maisha bali haimaanishi au atampa nafasi nyingine mtu aliyekosea. Hawaruhusu makosa hayo yatokee tena.

3. Hawafii kwenye Ugomvi 
Kitu kingine watu waliofanikiwa ni namna ya kutawala hisia zao, wanaweza kupuuzia ugomvi au vita ili wapigane siku nyingine. Kwenye ugomvi wowote unapotaka umalizane wakati huo huo ni rahisi kupata madhara makubwa au kusababisha hasara kubwa, hivyo kama mtu uliyefanikiwa unatakiwa kuchagua na kufanya maamuzi sahihi hata kama una hasira kubwa kiasi gani. Chagua kwa umakini na busara ni vita gani unatakiwa kupigana na kujua matokeo yake.

4. Hawaweki kipaumbele kwenye Ukamilifu
Watu hawa wanajua hakuna aliyemkamilifu hivyo hicho sio kitu cha kwanza kutafuta mkamilifu. Wanajua kuna kujaribu na kushindwa lakini wanaendelea kufanya juhudi kufikia mafanikio na sio kulalama kwenye maeneo walioshindwa.

5. Hawaishi kutakana na mambo ya zamani 
Kushindwa mara nyingi kunaondoa ujasiri fulani ndani ya mtu na inakuwa ngumu kuamini kama unaweza kufanya vizuri wakati mwingine baada ya kushindwa. Kushindwa kunatokana na kujaribu kufanya jamba ambalo si rahisi, kwahiyo watu waliofanikiwa wana uwezo wa kuinuka na kufanya vizuri baada ya kushindwa kitu fulani hivyo hawaishii kushindwa. Kinachotakiwa ni kuwa na moyo wa uthubutu kwa kila mambo. Usiruhusu kushindwa kusonga mbele.

6. Hawang’ang’anii matatizo
Pale matarajio yako yalipo ndio hisia zako zinakuwepo, kitu unachotakiwa kujua unapokua ndani ya matatizo unaanza kutengeneza hisia hasi na unapA msongo wa mawazo na kuathiri utendaji wako. unapoanza kuweka matarajio yako katika kuboresha na kuongeza utendaji wako inasababisha unaongeza hisia chanya katika mwenendo wako na utendaji wako. Watu waliofanikiwa wanachoangalia ni ufumbuzi wa tatizo na sio tatizo lenyewe.

7. Hawapendi kukaa na watu wenye mtizamo hasi 

Walalamishi si watu wazuri kwakuwa wanachongalia ni tatizo na kuendeleea kuongelea tatizo na kushindwa hivyo hawatafuti namna ya kutatua matatizo. Walalamishi wanataka watu waungane nao katika kulalamika ndipo wanajisikia vizuri. Kitu ambacho unatakiwa kujifunza je kama wewe hupendi sigara na huvuti sigara utakaa siku zjima na mvutaji sigara  huku ukiambulia moshi wake? Kwa mtu yeyote atamkwepa mvutaji huyo, hivyo hivyo na watu wenye mawazo hasi ni watu wa kuwakwepa kwani wanakuchafulia namna unavyofikiri na kuwaza.

8. Hawana Visasi na Uchungu
unaposhikilia na kuwa na uchungu wa muda mrefu kuhusu mambo fulani au mtu fulani unajikuna unatengeneza malipizi na visasi na mara nyingine kupata hapa msongo wa mawazo. Ukitaka kufanikia kwa gharama yoyote inabidi uondokane na visa na uchungu wa muda mrefu, ni kitu ambacho kitakusaidia wewe pamoja na afya yako itakuwa bora zaidi.

9. Hawasemisemi ovyo ovyo mpaka wawe na sababu ya kusema
Watu wengi waliofanikiwa sio waongeaji sana mpaka wawe na kitu cha kuongea. Na mara nyingi ni vigumu kusema hapana, lakini watu waliofanikiwa huwa hawapendi kupindisha maneno kama hawawezi kufanya watakwambia hakiwezekani. Ingawa watu wengi wanapendaa kuridhisha kila mtu kwa kusema nitajaribu au nitaangalia kwa mtu aliyefanikiwa hafanyi hivyo na hatakiwi kufanya hivyo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents