Habari

Mama wa mtoto aliyeteswa na mfanyakazi wa ndani asimulia, mfanyakazi afunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua

Mfanyakazi wa ndani ambaye video iliyosambaa mtandaoni inamuonesha akimpiga kikatili mtoto mdogo, amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.

https://www.youtube.com/watch?v=1EAKA_vkOp4&sns=tw

Jolly Tumuhirwe, mfanyakazi huyo wa ndani kwenye video hiyo anashikiliwa kwenye mahabusu ya gereza la Luzira, Kampala nchini Uganda na anatarajiwa kupanda kizimbani December 8.

Mtoto huyo kwenye video anaitwa Arnella Kamanzi ambaye pamoja na kuonekana mcheshi, anaendelea kukumbuka mateso aliyoyapata kiasi kwamba hakubali tena kubebwa na mtu asiyemfahamu.

arnella
Mtoto, Arnella Kamanzi

Kwa siku tatu hizi, mtoto Arnella mwenye miezi 18, amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, kutokana na video hiyo inayomuoneshwa akipigwa bila huruma na mfanyakazi huyo.

Mama yake, Angella Mbabazi bado anaendelea kuumizwa na walichokishuhudia kwenye video hiyo kiasi ambacho hulia kila anaposimulia. “Mfanyakazi mwingine alimpendekeza kwetu. Alituambia kuwa alikuwa anatokea kijiji cha Rukungiri. Ni baada tu ya tukio hili baya alituambia kuwa alikuwa mfanyakazi huko Nakulabye kabla ya kuja hapa,” aliliambia gazeti la Daily Monitor la Uganda.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kila alipokuwa akijaribu kujua historia yake, Tumuhirwe alikuwa akihama kochi na kuloa jasho na kutoa jibu la neno moja. Ms Mbabazi hakuweza kutambua alama za nyakati zilizoashiria hatari mapema na kujipa moyo kuwa siku moja msichana huyo angemweleza mambo yake.

Wakati siku zilivyoendelea kwenda, wazazi hao walikuwa wakirejea nyumbani kutoka kazini na kumkuta Arnella akichechemea, akiwa na majeraha na mikaruzo kibao. Sio mara moja na sio mara mbili, ni mara nyingi. Tumuhirwe alipoulizwa nini kimetokea, alikuwa akijibu kwa ufupi tu ‘Sijui’

“Kila tulipokuwa tukirejea nyumbani, tulikuwa tukikuta nyumba safi, angewaogesha watoto, kuwalisha na kuwapeleka kulala. Mtoto wetu wa kwanza huenda shule hivyo hakuna ambaye angetueleza chanzo cha mikwaruzo ya Arnella. Hapo ndipo tulipoamua kuweka CCTV cameras kwenye nyumba,” alisema.

Baada ya kuweka camera hizo, wazazi hao walibaini tena kuwa mtoto wao hakuwa sawa na ndipo walipoamua kuangalia footage na kukutana na unyama huo uliowaacha mdomo wazi.

Alipoulizwa kama anafikiria kuajiri mfanyakazi mwingine, Mbabazi alikosa cha kujibu na kuanza kulia huku akilala kifuani kwa mume wake. “Inaumiza. Siwezi kuelezea ninavyojisikia. Tuliamua kuiweka hiyo video kwenye mitandao ya kijamii ili kwamba wazazi wengine wajifunze,” anasema na kuongeza “Kwa neema za Mungu mtoto Arnella ni mzima. Alipewa matibabu na kupona. Yupo salama na Mungu alimlinda.”

Chanzo: Daily Monitor

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents