Habari

Malengo hubadilika lakini thamani yako haibadiliki, fahamu kwanini

Wakati wa kubadilisha malengo kuyapeleka kwenye uthamani, inawezekena ukasema malengo ndio jambo la msingi, inawezekana ni kutokana na makuzi uliyokuzwa. Mara ngapi umeulizwa swali hili “Je miaka mitano ijayo utakuwa wapi? kibiashara,au kielimu ama kikazi.

Mara nyingi tumekuwa tukiangalia wapi tunakwenda  bila kujali athari ya vitu tunavyofanya sasa. Hakuna kitu cha msingi na muhimu kitakachotokea ndani ya mwezi mmoja, namna utakavyojitoa sadaka leo ndio namna maisha yako ya baadaye yatakavyoboreshwa. Unapoangalia mbele zaidi inawezekana ukashindwa kuangalia na kuthamini yanayoendelea sasa.

Malengo ni muhimu. Malengo huleta mwelekeo  wa tunakokwenda na nini tunakitarajia kwenye maisha, lakini malengo hayo hayo hubadilika kulingana na mambo yanavyokwenda kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitaaluma. Malengo ni baraka na kutufanya kupata hamasa na kuwa na mwelekeo, hugeuka laana na kutufanya wakati mwingi kutoridhika na kile ulichonacho.

Confused woman

Inawezekana malengo yangu ni kukimbia mbio ndefu kwa muda mfupi sana, lakini kwanini nilianza kukimbia, kwanini nimeshiriki mashindano haya mara mbili mwaka uliopita. Je mashindano haya yameniongezea ujasiri na kuboresha afya yangu? Hivyo afya yangu ni muhimu kuliko kukimbia kwenyewe.

Kama nina malengo ya kuingiza fedha kiasi fulani kila mwezi, swali la kujiuliza je kazi ninayofanya itaingiza hizo pesa au Biashara ninayofanya? Je Biashara hii au kazi hii inanipa uhuru ninaohitaji, wapi nifanye kazi, nipate ninachotitaka, lini na mahali gani? Kama Biashara inanipa eneo kubwa la kufanya maamuzi na kujitawala hivyo basi kama ni uhuru kama mjasiriamali kwangu ni jambo la muhimu sana.

Kama sina jambo ambalo ninakusudia kwa kasi na fedha ninazotengeneza, sitakuja kuridhika na kile nilichonacho.

Malengo yatabadilika, wakati wote nikitaka kwenda benki kutoa hela zaidi nitakwenda kama mwenye wazimu nikijaribu kujiokoa kana kwamba nashindwa ili niendelee kufanya zaidi. Kama wateja wangu watafurahi kwa kile ninachowafanyia wakati huo huo familia yangu inahuzunika kwasababu sina muda wakutosha wakati wakinihitaji, nikifika mwisho familia yangu inahitaji umuhimu wa hali ya juu, lazima niangalie kwa upya malengo yangu.

Ukiangalia thamani, kitu ambacho utajali zaidi ni kujua kwanini unafanya hicho unachofanya ndipo utakapogundua kwamba umefanikiwa au la!

Leo nakushauri kubadilika kutoka kwenye malengo na kutazama thamani ya kile unachokifanya. Angalia thamani ya familia yako, maisha yako, uhuru wako, taaluma yako ndipo uanze kufanya maamuzi yako. Malengo hubadilika ila thamani yako haitabalika kamwe.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents