Habari

Malaysia Airlines kubadili jina baada ya ndege zake 2 kupatwa majanga ndani ya miezi 6

Kampuni ya ndege ya Malaysia Airlines inafikiria kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha biashara baada ya majanga yaliyozikuta ndege zake mbili ndani ya miezi sita mwaka huu na kuathiri biashara yao kwa kiasi kikubwa.

malaysia

Miongoni mwa mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na kampuni hiyo ambayo Sehemu kubwa ya hisa zake zinamilikiwa na serikali ya Malaysia ni pamoja na kubadili jina.

Mkurugenzi wa biashara wa kampuni hiyo, Hugh Dunleavy ameiambia The Sunday Telegraph kuwa serikali ya Malaysia tayari imeanza kutathmini hali ya baadae kibiashara kwa shirika hilo.

“Our majority shareholder, the Malaysian government, has already started a process of assessing the future shape of our business and that process will now be speeded up as a result of MH17.”

Janga la hivi karibuni kwa kampuni hiyo ni la ndege yenye namba MH17 iliyokuwa ikitokea Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur (July 17) , ambapo ilidunguliwa na kuanguka Ukraine na kudaiwa kusababisha vifo vya watu wote 298 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Janga la kwanza kwa mwaka huu lilitokea March 8 baada ya ndege ya Malaysia MH370 iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur ikielekea Beijing china kupotea ikiwa na watu 239.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents