Burudani

Malaika wa ‘Uswazi Take Away’ awataka wasanii wa kike kuiga mfano wa Vanessa Mdee

Muimbaji aliyewahi kushirikishwa na Chege kwenye wimbo wake ‘Uswazi Take Away’, Diana Malaika amewataka waimbaji wenzake wa kike nchini kuiga mfano wa Vanessa Mdee.

IMG-20150123-WA0010

Akizungumza na Bongo5, Malaika ambaye hivi karibuni aliachia wimbo uitwao ‘Mwantumu’ amedai kuwa Vanessa amekuwa ni mwanamuziki anayejituma na ndio maana amekuwa akikua kila siku.

“Unajua muziki kwa wasanii wa kike umekuwa na ushindani tofauti na zamani. Napenda tu kuwaambia wasanii wenzangu wa kike tupendane na tuwe na ushirikiano. Napenda sana kuiga mfano wa Vanessa Mdee. Alipoanzia hadi hapa alipo unaona kabisa ana mabadiliko,” amesema.

IMG-20150123-WA0011

Kwa upande mwingine, Malaika amedai kuwa hakuwahi kujijua kama anaweza kuimba.

“Unajua nilifanya vizuri sana katika wimbo ‘Uswazi Take Away’ nikaonekana kama msanii mzoefu. Sikutegemea kama ningekuwa bora kiasi hiki,” amesema muimbaji huyo.

“Uswazi Take Away’ndio ulikuwa wimbo wangu wa kwanza. Baada ya hapo ndIo nikatoa wimbo wangu mwenyewe unaitwa ‘Nenda’ video alifanya Adam Juma. Kuanzia hapo ndo nikaona sasa nifanye muziki serious na nitimize ndoto zangu maana nilikuwa napenda muziki tokea zamani ila kwakuwa wazazi waliniambia nimalize kwanza masomo ndio nianze muziki.”

“Sasa hivi nimeachia wimbo wangu mpya unaitwa ‘Mwantumu’ nashukuru mashabiki wameupokea vizuri na nategemea kutambulisha video ambayo nimefanya na Kwetu Studio, tarehe 1/2/2015 pale Maisha Club. Nitakuwa na wasanii wengine kama TID, Pam D, Mesen Selecta, Tunda Man, Linah, Matonya na Makomando.”

IMG-20150123-WA0009

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents