Malaika Mihambo: Mjerumani/Mtanzania aliyeikaribia medali ya dhahabu Olimpiki 2016
Inafahamika kuwa Alphonce Felix Simbu ndiye Mtanzania pekee aliyeibakiza ‘hivi tu’ aimiliki medali kwenye michuano ya Olimpiki iliyomalizika mjini Rio de Jeneiro, Brazil kwenye marathon.
Malaika Mihambo
Lakini kuna mwanamichezo mwenye damu ya Tanzania, mwenye CV moja matata sana aliyeinusa pia medali kwenye michuano hiyo.
Thanks, kwa AY kwa kunitambulisha kwa Malaika Mihambo, Mjerumani mwenye asili ya Tanzania. ‘Mihambo’ jina la kisukuma hili kutoka kwa baba yake.
Ni mrukaji wa umbali mrefu wa Ujerumani aliyezaliwa February 3, 1994. Alikamata nafasi ya nne kwenye fainali za long jumb kwenye Olimpiki, Rio 2016.
Well, pamoja na kuikosa medali ya Olimpiki mwaka huu, Malaika anazo kadhaa za mashindano makubwa.
Alishinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya vijana ya Ulaya mwaka 2013 na kushika nafasi ya nne kwenye mashindano ya Ulaya mwaka 2014.
Baba yake, Mihambo anatokea Zanzibar lakini msukuma wa Mwanza. Mama yake ndiye Mjerumani. Si wanasema mtoto hufuata utaifa wa baba? Sasa mbona huyu wa kwetu kabisa?
January 2014, alitajwa kuwa mwanamichezo kijana wa mwaka 2013 wa Ujerumani.