Habari

Makosa matano ya hatari unayopaswa kuepukana nayo unapoanzisha biashara

Uko tayari kuanzisha biashara au kuifungua hiyo biashara, na umenuia kufanya hivyo kwa shauku kubwa? Kuna mambo ya msingi ambayo inakubidi yakukae akilini wakati unafanya maamuzi ili kuepuka kupata matatizo badala ya maendeleo kibiashara.

o-HAPPY-BUSINESS-WOMAN-facebook

1. Kuchagua Mfanyabiashara mwenza ambaye unajua hamtaendana 
Baada ya kuanza biashara utakutana na watu wengi ambao wanataka kujiunga na wewe na hii kwa wakati mwingine ni kikwazo pia na wakati mwingine si nzuri. Inakubidi uangalie vigezo fulani kujua huyu mtu ni wa tabia gani na ujuzi gani ili uweze kulinganisha uwezo wake na biashara hiyo. Kama unafikiri hamtaendana usilazimishe mwendane achana naye.

2. Kuchukua mtaji wa kuanzia kutoka sehemu nyingine wakati hauhitajiki sana
Ukweli ni kwamba unaweza ukapata mtaji kutoka kwa mtu ambaye anaamini kwamba unaweza ukafanya kitu na biashara ikakua. Bali pale ambapo biashara inakwenda vizuri ndipo unagundua hukuhitaji mtaji wa mtu yeyote na hautakuwa na furaha ukigundua ya kuwa kuna mtu anamiliki asilimia 25 ya biashara yako kwakuwa ulichukua mtaji kwake.

3. Kubakia kwenye kazi yako ya kuajiriwa
Huwezi ukafanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Kama unaona uko tayari kujitegemea inakubidi utoke na ukajitegemee ili utumie muda wako wote kwenye biashara yako. Ingawa kuna watu wanafikiri wanaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, kama unawekeza hiyo inawezekana ila kama unaanzisha biashara wewe mwenyewe ni vigumu sana, hivyo usijidanganye inakubidi ufanye maamuzi ya msingi.

4. Unapoajiri mtu wa kwenye familia yenu au rafiki yako
Inawezekana shemeji yako anajua mahesabu vizuri au mtu uliyesoma naye anaweza biashara vizuri na wote wanatafuta kazi. Unaweza kujiuliza je wana ujuzi unaofaa kwaajili ya biashara? Wewe umejiridhisha kwamba wana uwezo wa kufanya kazi na wanaweza kufanya mambo makubwa lakini usiwaweke kwenye tegemeo la juu kwani utapata usumbufu mkubwa. Ingawa kama wanna ujuzi na uelewa wa bidhaa na huduma unayotoa hicho ni kitu kingine ila kama wapo wapo tu, usiwape nafasi hata kidogo.

5. Kununua vitu vingi vya kuanza navyo
Ni vizuri sana unapoaanza na vitu vingi na hata vitu vyenye teknolojia mpya kwenye biashara yako, lakini hebu fikiria kwanini usingetumia komputa au vifaa ambavyo ukonavyo kabla ya kuanza kununua vitu vipya? Achana na habari ya kupamba au kufanya ofisi yako ionekane nzuri zaidi, unahitaji kuingia gharama kwa vitu unavyohitaji na vya msingi tu.

Hivyo anza biashara lakini ingia kwa umakini mkubwa wa kujua kinacho faa na kisichofaa. Inakubidi ufanye maamuzi ya msingi na yenye nguvu ambayo yatajenga msingi mzuri wa biashara.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents