Habari

Makonda kuruka na orodha ya tatu ya vinara wa unga leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo anatarajia kutaja majina mengine ya vinara wanaotuhumiwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya.

Katika awamu ya pili, watu mashuhuri wakiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima na mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan walitajwa.

“Awamu ya tatu imekamilika naomba tukutane kesho katika ukumbi wa mwalimu nyerere kuanzia saa 4 asbh,” mkuu huyo wa mkoa aliandika jana kwenye Instagram.

Jana Rais Dkt John Magufuli aliwataka viongozi kuongeza nguvu kwenye mapambano ya biashara hiyo haramu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents