Habari

Makonda azijibu tuhuma zilizotolewa na Wema Sepetu kuhusu Masogange

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”

“Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.

“Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”

Majina 65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents