Burudani

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence atajwa kuhudhuria kwenye ‘Super Bowl 51′

Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence ameripotiwa kuwa atahudhuria fainali za Super Bowl 51 Houston, Marekani.

Endapo Pence atahudhuria kwenye tamasha hilo atakuwa makamu wa Rais wanne wa Marekani kuhudhuria baada ya Spiro Agnew, George H.W. Bush na Al Gore ambao wamemtangulia. Wasanii ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye fainali hizo ni pamoja na Lady Gaga, Hamilton, Luke Bryan na wengine.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Jumapili hii ya Februari 5 kwenye uwanja wa NRG Stadium ambao unachukuwa watu 72,220.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents