Habari

Majivu ya mwili wa Fidel Castro yazikwa Santiago, Cuba

Majivu ya aliyekuwa rais wa Cuba, Fidel Castro yamezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.

_92826498_fidelasshes

Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti. Jumapili hii rais wa Cuba, Raul Castro, amesema serikali yake itakataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.

Huku akiongeza kuwa mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu. Fidel Castro amefariki dunia akiwa na miaka 90.

BY: EMMY MWAIPOPO

CHANZO: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents