Burudani

Majirani wa anapohamia Justin Bieber, Atlanta wapanga kuandamana kudai hafai kwa watoto wao

Ukorofi wa Justin Bieber sasa unapelekea awe tishio la watu wengi hususani wazazi ambao wanaogopa kuwa kwake karibu na watoto wao anaweza kupelekea kuwaharibu kitabia.

bieber

Mwimbaji huyo wa Canada Bieber (19) anatarajia kuhamia makazi mapya huko Atlanta alipopanga kwenye nyumba ya rapper Dallas Austin, na badala ya majirani kufurahia kupata jirani star, wamepanga kuandamana kupinga Bieber kuhamia eneo lao sababu wanahofu anaweza kuwaambukiza tabia mbaya watoto wao.

Kwa mujibu wa TMZ wakazi hao wa Buckhead, Atlanta wamepanga kuandamana leo Jumatatu, na zaidi ya wakati 200 wa eneo hilo wamethibitisha kushiriki kwa kusaini ‘petition’ inayosomeka:

“Tumefanya kazi kubwa kufikia malengo yetu na kufika hapa tulipo, kuhamia kwa Justin Bieber Atlanta ni mbaya kwa watoto wetu. Wengine wanashindwa kuwaacha watoto wacheze bila uwogo, amekuwa akikimbiza magari hapo nyuma…Tafadhali usiruhusu mtoto aharibu tulichofanyia kazi kwa bidii kukipata”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents