Burudani

Majina ya tuzo za MTV Africa ‘MAMA’ kutangazwa leo

Mastaa kibao kutoka nchini mbalimbali barani Afrika wapo jijini Johannesburg ambako leo Jumatano ya April 16 majina ya wasanii watakaowania ‘2014 MTV Africa Music Awards KwaZulu-Natal (MAMA)’ yatatajwa.

Mwimbani wa kundi la Mafikizoro Theo Kgosinkwe akifanya wako
Jumla ya vipengele 14 vitashindaniwa mwaka huu ambavyo ni pamoja na Best Male, Best Female, Song of the Year, Artist of the Year, Best Group, Best Lusophone, Best Francophone, Best Hip Hop, Best New Act, Best Live, Best Pop, Best Alternative, Best Collaboration na Best International.

Wasanii watakaokuwepo kwenye hafla ya kutajwa majina hayo ni pamoja na AKA (South Africa), Mafikizolo (South Africa), Professor (South Africa), Oskido (South Africa), Burna Boy (Nigeria), DJ Clock & Beatenberg (South Africa) na Yuri Da Cunha (Angola).

Pamoja na tuzo za muziki, mwaka huu MAMA itakuwa na vipengele vitatu vya mambo ya maisha ambavyo ni Personality of the Year, MTV Base Leadership Award na Transform Today by Absolut.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents